Monday, September 18, 2017

AFRIKA YA KESHO. MTU AKIKUAMBIA UJINGA NI BORA KULIKO USTAARABU USIMSADIKI

 Makala hii itamfanya mtu yeyote atayoisoma kwa makini na utulivu, atayeisoma bila papara, kukaa chini na kutafakari tulipotoka, tulipofika, na tunapoenda. Makala hii Iliandikwa mwaka 1923 na mwandishi ambae hakujitambulisha. Hapa kuna mengi ya kujifunza na maswali mengi zaidi ya kujiuliza leo hii, miaka karibu 100 tangu makala ichapishwe. Ustaarabu ni nini? Tulikuwa vipi kabla ya wageni?Tumetoka wapi, tupo vipi sasa hivi, na tunaelekea wapi?
AFRIKA YA KESHO. MTU AKIKUAMBIA UJINGA NI BORA KULIKO USTAARABU USIMSADIKI 

Tangu zamani, kabla Wazungu hawajaja katika inchi yetu ya Afrika, sisi tulijifahamu wenyewe kuwa ni watu wa nyuma sana, yaani si wastaarabu. Watu wa inchi zingine walikuwa watuwastaabika. Na sisi asili ya kukosa kustaarabu ni hii:
sisi siku zote tunakimibilia ganda la ustaarabu, asili ya ustaarabu tunaiacha. Mfano kama hivi.
Katika kufafanua kwetu macho tumewaona Waarabu ndio wastaarabu wa kwanza tuliowaona katika inchi yetu. Wakaja na ustaarabu wao wakakaa miaka kathawakatha. Na ingiwa wao hawakutaka sisi tustaarabu, lakini kwa kukaa nao tu tungeweza kuiga ustaarabu. Lakini tutazame tumeiga nini kwao? Hakika tukiwa tunataka tuwape haki yao wameleta dini katika inchi ya Afrika, na kwa dini yao watu kidogo wamekuwa hawajambo kwa mambo mengine ya desturi za ustaarabu. Lakini zaidi kuliko hivi hatukuiga neno illa mambo yasiyo na faida. Kununua watumwa, kujaribu kuwatuma wenzetu watufanyie kazi, sisi wenyewe tuvae joho na vilemba, na mambo kama haya.
Na Zaidi kuliko haya tukawatwaa ndugu zetu tukawauza kwa Waarabu, wengine wakawahadaa tu kwa kuwapa kanzu na kuwachukua pwani. Tena tukatwaa mali yetu tuliokuwa nayo ya pembe tukawauzia wao kwa doti ya shuka. Wao wakachukua mali na ndugu zetu, wakaenda zao Maskati, Unguja, na Pemba, wakanunua mashamba wakastarehe. Sisi wakatuacha na ujinga wetu. 
Hatima imekuja Dola ya Kizungu, na Wazungu kama tujuavyo wanataka sana tustaarabu, yaani tuwe watu kama watu. Lakini naona tumeanza kufanya makosa yale yale tuliofanya wakati wa Waarabu, ya kuchukua maganda ya ustaarabu, kuacha ustaarabu wenyewe. Nyinyi wenyewe mnaona yakuwa siku hizi vijana waote wanakimbilia wanaoita ustaarab wa Kizungu, kuiga mwendo wa Kizungu, kusema kwa sauti ya Kizungu na mambo mengine kama haya ambayo hayamfai mtu kwa lolote. Na sisi twajiona tumestaarabu, kumbe ni ujinga.
Ustaarabu ni nini? Ustaarabu ni kuwa watu kama watu. Yaani kuendelea katika mambo yote ya dunia yanayotuletea faida sisi na inchi yetu. Huu ndio ustaarabu. Tujitahidi kuendelea katia (1) Mambo ya Biashara, (2) Kazi ya Ufundi, (3) Kusoma, (4) Kulima, (5) Ukarani, 
Labda mtaniuliza kuwa kwani sasa hatufanyi hayo? Tunafanya, lakini hatufanyi kama inavyopasa. Mambo haya yote yanafanywa na wageni, yaani watu wa Asia, wanafanya haya yote wanapata mapesa wanarudisha kwao, sisi wnatuacha na ujinga wetu.
Ingekuwa ni watu wa kuamka, na kushika ustaarabu, tangu kuja Wazungu katika inchi yety tungalikuwa tumeanza kuonyesha alama za ustaarabu. 
ITAENDELEA!



No comments:

Post a Comment