Mwalimu alikuwa rafiki wa Raisi wa Marekani John F. Kennedy. Viongozi hawa wawili walikutana mara kadhaa; walikutana mwaka 1961 kabla Tanganyika haijapata uhuru. Mwalimu Nyerere na raisi Kennedy walifanya walikutana kwa maongezi Julai mwaka 1963. Mwalimu alisikitishwa sana na kifo cha raisi Kennedy kilichotokea Novemba 22 mwaka 1963. Alimuandikia barua ya rambirambi mkee wa raisi Kennedy, Jacqueline Kennedy. Mama Jacqueline Kennedy alimjibu Mwalimu Nyerere na barua hii Februari 1, 1964.